GET /api/v0.1/hansard/entries/1490853/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1490853,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1490853/?format=api",
    "text_counter": 168,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "kampuni kwa sababu kampuni zenyewe, hazina njia ya kupata fedha za kuwawezesha kukua. Jambo jingine ni kutegemea misaada ya mashirika ya kimataifa kwa swala la maji. Ijapokua ni wafadhili wetu na wanatusaidia, imekua sasa ni lazima sisi tujisimamie. Haiwezekani kuwa maji ambayo watu wa Mombasa wanapata yanatoka kwa Coast Water Services Board ambao wanauzia shirika la Mombasa Water na pia wanapewa muda wa kulipa, kama siku 90 au 100. Hiyo ni credit window ambayo inatumika. Hii pia haisaidii. Utapata kwamba maji yanapofungwa, inabidi watu wapigiane kelele na kukumbizana ili maji yafunguliwe na wananchi wapate maji. Mbali na kuleta ripoti hii, Kamati iangalie kwa ndani vile tunaweza toa hizi kampuni zijinasue na lindi hili la ukiritimba unaosababisha wananchi kukosa maji na kampuni zisikue. Bw. Spika wa Muda, kuna haya mashirika ya serikali kama Coast Water Services Board, Tana Athi Water Works Development Agency na Lake Victoria North Water Services Board na kaunti zetu zinatakikana zipewe hisa katika mashirika haya. Lisiwe ni shirika la serikali kuu na wanapeana maji. Ukiangalia kama wale wakurugezi waliochaguliwa, hawana uzoefu katika maeneo yale. Kwa hivyo, inakua ni vigumi kuleta mawazo na fikra ambazo zitakusaidia kurekebisha zile kampuni. Kwa mfano, kwa shirika la Coast Water Services Board, serikali inaweza kua na hisa moja na kila kaunti ya Kwale, Mombasa, Kilifi, Tana River na Lamu ipewe hisa moja; ili wao pia wawe na uwezo wa kusikiliza maswala yao katika mashirika hayo. Kwa hayo mengi, naunga mkono ripoti na kuipongeza Kamati hii kwa kazi nzuri inayofanya, ikiongozwa na kiongozi wetu, Sen. Osotsi ambaye pia ni naibu kinara wa chama chetu cha ODM. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}