GET /api/v0.1/hansard/entries/1491304/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1491304,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1491304/?format=api",
    "text_counter": 75,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa mbili; moja ya kifo cha dada Victoria Mumbua ambaye alikuwa dereva wa taxi kule Mombasa. Kifo chake kilisikitisha wengi sana ikikumbukwa kwamba dada huyu alikuwa akifanya kazi yake ya halali ili kukidhi mahitaji yake na ya watoto wake wawili. Wakati nchi yetu inaingia katika himaya ya biashara ya masaa 24, bado hatujaweza kuhakikishia usalama wale wanaosaidia pakubwa kuendesha biashara hii. Tukizingatia, utaona kwamba wanaoendesha taxi wanafanya hiyo masaa 24. Hii ni kwa sababu biashara yao inafanyika kinyume na yale masaa ya zamani. Ni lazima Serikali ihakikishe kuwa usalama wa watu hawa unazingatiwa ili waweze kuendesha biashara zao bila matatizo. Taarifa ya pili ni ile ya uchaguzi wa Football Kenya Federation (FKF). Kwa muda mrefu sasa, FKF imekuwa kama donda sugu katika nchi yetu. Kumeletwa taarifa kadhaa katika Bunge hili na tukafanya uchunguzi katika Kamati ya Leba lakini hadi sasa, mambo haya hayajatatuliwa. Kumetengenezwa jopo la kusimamia uchaguzi huu ila jopo hili limechaguliwa na rais wa FKF anayeondoka. Rais huyo pia ni mgombea kwa sababu amempendekeza yule makamu wake wa miaka minane iliyopita awe Rais kisha yeye awe naibu wa rais. Hiyo ni kesi ya kumpeleka mbuzi kwa fisi kwa sababu lazima atachukua hatua za kuhakikisha kwamba jopo lake limechaguliwa katika kuendesha FKF kwa muda mwingine wa miaka minne. Bw. Spika, sheria ya michezo nchini kwetu inasema kwamba wasimamizi wa vitengo mbalimali vya michezo watahudumu kwa muda wa mihula miwili ya miaka minne. Huyu anataka kujiregeshea muhula mwingine wa tatu, nne, tano na sita kama alivyofanya Mhe. Rais Putin kule Urusi. Kwa hivyo, ni lazima suala hili liangaliwe mapema kwa sababu hatutaki masuala kama haya yarejee katika mahakama. Yaweze kwenda na kurejesha wakati nchi yetu inapoteza katika masuala ya michezo. Itakumbukwa kwamba kuguza FKF ni kama kuguza"
}