GET /api/v0.1/hansard/entries/1491434/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1491434,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1491434/?format=api",
"text_counter": 205,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika, nakushukuru kwa hekima na ubunifu wako wa utunzi wa sheria. Tukibadilisha hii sheria ya the County Public Finance Laws (Amendment) Bill (Senate BillsNo.39 of 2023), bunge za kaunti zitapata uhuru wake. Pesa nyingi huenda kwa magatuzi na kusipokuwa na bunge za gatuzi zinazofanya kazi vizuri, pesa nyingi hupotea, na wananchi nyanjani hawapati maendeleo ipasavyo. Mwaka wa 2010 tulijipatia Katiba iliyoleta ugatuzi. Hii ilimaanisha kwamba pesa zitoke Serikali kuu na kuenda mashinani, lakini magavana wameendelea kunyanyasa bunge za kaunti. Kwa mfano, mwaka wa 2021 nilikuwa katika Kamati ya Uhasibu ya Seneti na bunge za kaunti zingine hazikuwa zinalipwa mshahara moja kwa moja bali wanalipiwa na executive . Kwa bunge za kaunti kupata fedha zao, inabidi waziri wa fedha aandikie CoB ili awatumie zile pesa. Bunge zetu zimeendelea kupata shida kufadhili miradi na mipango yao. Kuna jambo lilitokea mwaka wa 2021 ambapo bunge limetengeneza makaratasi yake ya pending bills, lakini waziri wa fedha wa executive hawajatengeneza makaratasi ya kupeleka kwa CoB ili pesa irudi. Kwa hivyo, bunge za kaunti zinakawia kupata pesa kwa sababu inacheleweshwa na serikali ama executive . Kama wangekuwa na uhuru wao, pesa zao hazingechelewa kufika kwa bunge za kaunti. Jambo lingine litakalosaidia uhuru wa bunge za kaunti ni kwamba saa zingine hazina ya kitaifa inachelewa kutoa pesa na inabidi kaunti zikope pesa kutoka kwa benki. Bunge za kaunti hazijapewa uhuru wa kukopa kutoka kwa benki ili kulipa wafanyakazi wao bila kupitia kwa waziri wa fedha wa kaunti. Bunge za kaunti zikipata uhuru wao wakati hazina ya kitaifa imechelewa kutoa pesa, basi mabunge haya yatakuwa na uwezo wa kukopa pesa kutoka kwa benki ili kulipa mishahara. Nimekuwa nikinena kuhusu mambo mawili ambayo yanafaa yafanyike ili mabunge ya kaunti yafanye kazi vizuri. Jambo la kwanza ni kuhusu kuwepo hazina yao ndogo. Bw. Naibu Spika, katika Mswada wako, umesema kando na hazina ya kaunti kuwe na hazina ndogo ya mabunge ya kaunti ambayo itawekwa pesa ili bunge za kaunti zitumie pesa zao moja kwa moja. Bw. Naibu Spika, hata zile pesa zikiwekwa kwenye mabunge ya kaunti, gavana anaweza kukataa kufanya maendeleo kwa wadi . Tukipitisha Mswada huu, ule Mswada mwingine ambao lazima tuuangalie kwa karibu ni Mswada wa fedha yaani WardEqualisation Fund ili pesa zikifika kwa gatuzi kila kata ipate pesa zake na wapate kufanya maendeleo yao. Vile ilivyo hivi sasa, kama mwakilishi wa bunge la kaunti haimbi wimbo wa gavana, hatapata maendeleo kwenye eneo lake, ili wananchi wakasirike na yeye na wamnyime kura katika uchaguzi unaofuata. Haya mambo mawili ya kupatia mabunge ya kaunti uhuru wao na pia Mswada ule mwingine wa kupitisha Ward Development Fund yatasaidia wawakilishi wa bunge la kaunti kufanya kazi vizuri zaidi. Kifungu cha 109(e) kuna msemaji amesema si vizuri kupea waziri jukumu la kutoa fedha katika hazina ya kaunti. Natofautiana na yeye kidogo kwa sababu katika hazina ya kitaifa, waziri wa fedha ndiye anayeweka sahihi kwenye ugavi wa pesa kwa mahakama, bunge na taasisi mbalimbali. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}