GET /api/v0.1/hansard/entries/1491448/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1491448,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1491448/?format=api",
"text_counter": 219,
"type": "speech",
"speaker_name": "The Senate Minority Leader (",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Sen. Madzayo): Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Mswada huu. Kwanza, ningependa kutoa kongole kwako kwa sababu wewe ndiye ulileta Mswada huu kuhusu sheria za pesa za umma zinazoenda kwenye kaunti zetu, licha ya kuwa Mswada huu ni wa mwaka wa 2023 ilhali tuko katika mwaka wa 2024. Kama ungeuleta mwaka wa 2022, tungepata mwelekeo mzuri lakini hatujachelewa. Barabara iko wazi na tutaendelea vivyo hivyo. Sheria hizi zitasaidia Bunge hili. Mara nyingi, MCAs ndio wa kwanza kukumbana na shida za wananchi. Wakienda nyumbani kwao, ofisini ama wakiwapata barabarani, wao ndio watu wa kwanza kutatua shida za wananchi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}