GET /api/v0.1/hansard/entries/1491449/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1491449,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1491449/?format=api",
    "text_counter": 220,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The Senate Minority Leader (",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Si vyema kwa sababu mshahara wa MCA ni mdogo. Pesa zisipopelekwa katika kaunti zetu kwa wakati unaofaa, mara nyingi huwa kuna shida kwa sababu hawana la kufanya. Nafurahi kwamba tunajadili Mswada huu. Itafanya Mabunge ya kaunti zetu kuwa huru. Wakiwa huru, kutakuwa na mijadala mingi ya maana kule. Mara nyingi, MCAs wanaogopoa kuongea kwa sababu wanajua kuwa wakisema kitu fulani wanaweza kuchukuliwa hatua na serikali za kaunti. Ningependa kuwapa imani kwamba hivi karibuni sheria itapatikana. Kwa hivyo, watakuwa huru kuongea wanavyotaka wakiona kuna makosa. Bw. Naibu Spika, kwa kumalizia, ningependa kuzungumzia pesa ambazo zitakwenda katika kaunti zetu. Umefanya vizuri kupendekeza kuwa Mdhibiti wa Bajeti, yaani Controller of Budget (CoB), awe na uwezo wa kukagua pesa zote zitakazokwenda kwa mabunge ya kaunti. Anafa kusema iwapo kuna makosa ama jambo lolote ambalo haliendi sawa. Pesa hizo zitasaidia watu katika serikali za kaunti. Kwa hivyo, zitahitaji kuangaliwa vizuri ili kuhakikisha kuwa matumizi yake yanafanywa kulingana na sheria baada ya kuidhinishwa na Mdhibiti wa Bajeti, yaani CoB. Tukiwa na sheria hii, litakuwa jambo la kufaa zaidi. Nitakomea hapo, Bw. Naibu Spika."
}