GET /api/v0.1/hansard/entries/1491491/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1491491,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1491491/?format=api",
    "text_counter": 262,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sifuna",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13599,
        "legal_name": "Sifuna Edwin Watenya",
        "slug": "sifuna-edwin-watenya"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, kwanza, sisi wakaazi wa Nairobi tunazidi kutamaushwa sana na matukio haya kwa sababu visa vingi vinavyotendeka katika kaunti hii vinahusu wakaazi wa Nairobi. Huyo dada aliyeitwa Waris Dahabo Daud, mwanawe Amina Dahir na mpwa wake Nusayba Abdi walikuwa wakaazi wa Nairobi. Willis Ayieko pia alikuwa mkaazi wa kaunti hii, kama Sen. Kibwana alivyothibitisha kuwa alikuwa jirani wake. Ni Victoria Mumbua pekee aliyekuwa dereva wa taxi kule Mombasa ambaye mwili wake ulipatikana kule Nakuru. Yule dada mdogo aliyejulikana kama Seth Nyakio aliuwawa maeneo ya Thika. Juzi, dada mmoja aliyeitwa Lilian Muhavi alipatikana amenyongwa na mwili wake kutupwa kando ya barabara ya Naivasha kule Kawangware hapa jijini Nairobi. Kuna dada mwingie aliyeitwa Vivian Kajaya, mkazi wa Nairobi kule Kawangware. Mwili wake ulipatikana umetupwa Nakuru baada ya kuuawa. Bi. Spika wa Muda, ninavyokuhesabia visa hivi vilivyotokea katika majuma machache yaliyopita, hao ni wanadamu zaidi ya wanane ambao walipatikana. Hao ni baadhi tu ya walioripotiwa katika vyombo vya habari. Hatujui kama kuna wengine ambao kesi zao hazijaangaziwa na vyombo vya habari. Hiyo inaonyesha kuwa kuna genge la watu ambao wana uwezo wa kumchukua mtu kwenye barabara katika jiji hili na kumtendea unyama ambao tumeona dada na ndugu zetu wakitendewa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}