GET /api/v0.1/hansard/entries/1491492/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1491492,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1491492/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sifuna",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13599,
"legal_name": "Sifuna Edwin Watenya",
"slug": "sifuna-edwin-watenya"
},
"content": "Hata MCA wa Wajir County, Mhe. Yusuf Hussein Abdi, alichukuliwa akiwa kwenye barabara za Nairobi. Sisi kama viongozi wa Nairobi, tutazidi kusisitiza kwamba asasi zetu za usalama lazima ziwajibike ili kutoa majibu kwa familia hizi na pia kuonyesha wakaazi wote wa Nairobi kwamba kuna usalama wa kutosha ili kuhakikisha kuwa watu wanaishi kwa amani. Bi. Spika wa Muda, tulipozungumzia swala hili mapema leo adhuhuri, kuna dada zetu waliokuwa wanatoa pingamizi kwamba labda tunasema sio swala la kina mama pekee kuuawa. Kusema kweli, takwimu zinaonyesha kwamba wengi wa walioathirika na visa hivyo ni kina mama na hatujakataa. Hata hivyo, naamini kwamba hakuna aliye salama hadi sisi sote tuwe salama. Ndio maana nilipopata fursa ya kuketi na Inspekta Jenerali wa Polisi, Bw. Douglas Kanja, wengine waliniuliza kwa nini sikuwa naketi na Bw. Koome. Mnajua uhusiano wangu na aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi, Bw. Koome. Koome alikua ananiandama kama mnyama, mimi pamoja na Kiongozi wa Waliowachache, Mhe. Stewart Madzayo. Tumeona kifo na macho yetu chini ya mkono ya Koome. Mimi singeweza kufika kwenye ofisi ya Koome na nafurahi alituondokea. Tunaomba huyu ndugu yetu, Douglas Kanja, awe tofauti na Koome kwa sababu serikali hii ilhaidi kwamba, chini ya uongozi wa Dkt. William Ruto, haya matukio yatakuwa matukio yaliyopitwa na wakati. Tulikuwa Kaunti ya Vihiga na Mhe. Osotsi. Inawezekanaje wakati huu wote tunajua kwamba watu wanauwawa na miili yao kupatinaka katika mpaka wa Kaunti ya Siaya na Vihiga? Hatuwezi kuweka patrols za polisi katika mpaka huo? Kila wakati, miili inapatikana katika mto ulioko kwenye mpaka huo. Itawezekanaje jeshi la polisi haliwezi kuchuka hatua kwamba maeneo ambayo yanajulikana wazi kama matimbo na maeneo mengine ambayo mili ni kawaida kupatikana, kuwa na surveillance ya kutosha kuhakikisha kwamba mambo haya hayaendelei? Nitazidi kuongeza sauti yangu kwa ajili ya haki kupatikana kwa familia hizi. Kama nilivyosema hapa mchana, nilipoenda makafani ya City, ungeona hali ya miili ya Dhahabu na mwanaye, ulikuwa katika hali mbaya sana. Hii inamaanisha kwamba walipitia kifo cha uchungu sana. Hata zile ripoti ambazo tumepata kuhusu mwili wa ndugu yetu, Willis Ayieko ulivyokuwa, inamaanisha kwamba alipitia mambo magumu sana kabla ya kuaga dunia. Swali ambalo tunajiuliza ni kwamba, kwa sababu operesheni kama hio inachukua muda sana, inawezekanaje kwamba umuweke mtu mahali kwa wakati huo wote na kumkata kama kuku ama kumchinja---"
}