GET /api/v0.1/hansard/entries/1491503/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1491503,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1491503/?format=api",
    "text_counter": 274,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bi. Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kutoa rambi rambi zangu kwa familia, jamii na marafiki wote wa hizi familia ambazo zimeathirika kwa wapendwa wao kuuwawa katika hali ya kinyama na sintofahamu. Pia, ninatoa heko kwa ndugu yangu na mdogo wangu, Eddy, kwa kuwasilisha Hoja hii ambayo imeleta msisimko mpya ndani ya Bunge letu la Seneti. Tumeona Wakenya wanauwawa kiholelaholela na bila sheria na bila hatua yeyote kuchukuliwa na polisi. Kitu cha kwanza ningependa kutafakari vizuri ni kwamba, kuua watoto wadogo, tena watoto wa kike; watu ambao hawezi hata kupigana ama kujiregeshea ngumi au kusukuma mtu. Wewe unaenda unapata watoto wa kike wameketi mahali, ama kwao nyumban au wako barabarani; halafu mnawashika kwa nguvu na kuwaingiza ndani ya gari ama, mnawadaganya na mnaenda nao mahali fulani halafu hapo panapatikana na vifo. Bi. Spika wa Muda, hilo ni jambo la uchungu kuona watoto ambao hawawezi kujitetea wanapatikana katika hali hiyo. Kitu cha kukemewa zaidi ni kwamba watoto hao wapatikana sehemu zao za nyeti haziko, macho na matiti hayapo. Ni hali ya kinyama kiasi gani kwamba Mkenya, hata kama wewe ni jangili au muuwaji unaweza kumkata matiti na sehemu zake za nyeti mama ambaye hawezi kujisadia? Wewe ni binadamu wa namna gani? Kitendo kama hiki ni cha kukemewa na Wakenya wote. Kitu cha kushangaza ni kwamba, sisi tuna watu wanaopelekwa shule Kiganjo. Hawa ni polisi ambao wamesomea kulinda mali, haki na uhai wa watu. Katiba inasema uhai wa kila Mkenya utalindwa na Serikali. Hawa polisi ninauliza wako wapi? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}