GET /api/v0.1/hansard/entries/1491508/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1491508,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1491508/?format=api",
"text_counter": 279,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Sen. Sifuna anasema amebeba. Sikuona mimi. Nasema tu ya kwamba ni jambo la kusikitisha hivi leo ikiwa mtu mzima kama yule, aliyekuwa hana ubaya na mtu anaweza kupoteza maisha yake kiholela namna ile halafu anatolewa macho. Hata kama ni uhalifu, umefikaje kiwango hiki? Mwisho, huyu Inspector-General wa Polisi, Bw. Kanja, tuliyemchagua hivi majuzi, ninataka kumwambia aamke kutoka kwa huo usingizi; aamrishe askari wake wafike kila mahali. Vile vile, vitengo vingine vya uchunguzi kama vile Kitengo cha Ujasusi wawape wananchi ripoti za ujasusi na hatua zilizochukuliwa. Tunakemea sana. Lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya wahalifu hao. Hoja hii ambayo imeletwa na ndugu yangu, Sen. Oketch Gicheru, naomba tuichukulie kwa uzito mwingi sana. Asante, Bi. Spika wa Muda."
}