GET /api/v0.1/hansard/entries/149254/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 149254,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/149254/?format=api",
"text_counter": 520,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Mimi nitachukua muda mchache kwa sababu naona wakati umeenda ili Mwenyekiti aweze kuchangia kwa kufunga. Jambo hili ni ngumu sana na limezungumziwa sana. Ningependa kusema kwamba ingelikuwa ni jambo la maana sana kwa hii Ripoti kutiliwa maanani kabisa. Hii ni kwa sababu kidumbwe dumbwe cha taabu zilizoko magerezani ni kukosa mwelekeo. Mwenyekiti wetu ni shahidi wangu nikisema alipofungwa gerezani hakuwa na kazi ya kufanya. Ukimwangalia kwa makini utamwona ni kibonge cha mtu ambaye anangefanya kazi ya kuisaidia Serikali hii. Haikuwa jambo la busara kumfungia ndani ya jela bila kazi. Pengine kama angefanya kazi angeiletea nchi hii faida kubwa sana."
}