GET /api/v0.1/hansard/entries/149255/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 149255,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/149255/?format=api",
"text_counter": 521,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Mahabusu wa Uchina husambazwa kote ulimwenguni kufanya kazi ya ujenzi wa barabara. Wao hawaigharimu Serikali yao gharama yote kama vile kupewa madawa na chakula bila kufanya kazi. Wafanyakazi wa kampuni nyingi za kujenga barabara kutoka China huwa ni wafungwa. Kwa hivyo, badala ya kuwajaza mahabusu wetu katika miji mikubwa na kuwalisha bila kufanya kazi, ni lazima tuwahusishe katika ujenzi wa taifa. Tunajua taifa hili letu ni maskini sana. Hatuwezi kuendelea kuwapa chakula watu walio huru na pia mahabusu. Wafungwa hawa tunawapa dawa, malazi, maji na kila kitu. Ingelikuwa ni jambo la maana kama watu hawa wangelima mashamba yetu kule Tana River, Lamu na sehemu zingine. Haifai mashamba hayo kupewa wageni ilihali tuna wafungwa wa kutosha kufanya kazi. Kwa mfano, wafungwa 20,000 wanaweza kufanya kazi nzuri sana. Ukiwapa ekari 20,000, kila mfungwa atakadiriwa kufanya kazi katika ekari moja. Tukifanya hivyo, tutapata chakula cha kutosha hapa nchini na kuwapa wagonjwa wetu katika hospitali zetu. Jambo hili litachangia pakubwa kuokoa mamilioni ya pesa za Serikali zinazotumika kuwalisha hawa watu."
}