GET /api/v0.1/hansard/entries/149259/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 149259,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/149259/?format=api",
    "text_counter": 525,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ripoti hii inaonyesha kuwa kuna watu waliohukumiwa kifo. Wengi wao wanaomba msamaha. Wanajisikia kwamba wamebadilika na kuwa watu wazuri. Hukumu ya kifo inazungumzia katika vikao vingi na nina hakika kuwa litaletwa hapa Bungeni. Sheria ambazo tunabuni sasa zinabatilisha sheria za hapo awali. Ni dhahiri ya kwamba, hata Mungu hawapendi wauaji. Kwa hivyo, wale ambao wanaua watu wengi wasifikirie kwamba watasamehewa kuambatana na sheria zetu. Kuna baadhi ya watu wanaofikiria kwamba wakiua watasamehewa kufuatana na miswada inayojadiliwa Bungeni. Kabla ya miswada hiyo kupitishwa, bado wanaendelea kuua wakitarajia kusamehewa. Wafungwa wengi wamezungumza sana kuhusu shida zao. Ikiwa Serikali inaweza kuwalipa vizuri mahakimu na majaji, basi tunaweza kuwaajiri wengi ili kuchunguza upya hukumu za wafungwa wetu katika jela zetu. Ni aibu kuona jaji au hakimu mmoja anasikiliza kesi nyingi kwa siku. Ni vigumu kwake kuweza kutoa uamuzi mwafaka katika kesi hizo sote. Je, atasikiliza kesi wakati gani na kutoa hukumu? Ingekuwa ni vizuri kwa Serikali yetu kuwaajiri mahakimu wengi. Ni lazima tuwe na majaji wa kutosha katika wilaya zetu. Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Ripoti hii."
}