GET /api/v0.1/hansard/entries/1493748/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1493748,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1493748/?format=api",
    "text_counter": 185,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Laikipia North, JP",
    "speaker_title": "Hon. Sarah Korere",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": " Shukrani, Mhe. Spika wa Muda. Nakubaliana na ndugu yangu, Mohammed Adow. Pia, namsikitikia sana mwenzetu aliyejaribu kujibu hilo swali kwa niaba ya idara husika. Nimesikiliza majibu yake na ni ya kukasirisha kidogo. Ukweli ni kwamba kuna fedha taslimu ambazo zimeachwa katika idara hii ili kushughulikia maneno ya sehemu kame katika kukuza chakula ili tusiwe watu wa kuombaomba. Saa zingine, watu wetu wanawekwa kwa aibu. Kila siku wanasimama na gunia kungoja kupewa kilo moja au mbili za mahindi. Majibu waliyopeana yanakera sana na haina msingi yeyote. Saa zingine pia, wenyeviti wa kamati wawe waangalifu wasije wakadhalilishwa na hawa mawaziri kwa kupeana majibu kiholelaholela ambayo hayajibu chochote ambacho kimeulizwa. Ahsante, Mhe. Spika wa Muda."
}