GET /api/v0.1/hansard/entries/1494205/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1494205,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1494205/?format=api",
    "text_counter": 642,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii nichangie mambo yanayohusu nafasi za kazi katika nchi yetu ya Kenya. Kwanza, ningependa kumshukuru Chairman wangu aliyeleta mjadala huu katika Bunge jana. Ripoti hii ilisikilizwa sana na Wajumbe waliokuwa ndani ya Bunge wakati huo. Ningependa pia kuipongeza Kamati yangu ya National Cohesion and Equal Opportunity kwa kufanya kazi kubwa ya kutengeneza Ripoti hii iliyoletwa Bungeni jana. Kamati iliamua kuchunguza kinachoendelea katika Wizara mbalimbali kuhusiana na mambo ya nafasi za kazi. Tulipoanza uchunguzi, tulikutana na Wizara 18. Baada ya kufanya mikutano nao na kuuliza sababu ambazo zimepelekea kabila zingine kukosa kazi, walitaja mambo mengi sana. Mengine yalihusiana na namna taarifa hufikia wananchi mashinani. Kuna watu wanaokaa sehemu fulani, na inakuwa vigumu kwao kujua kinachoendelea nchini Kenya, hususan mambo ya nafasi za kazi. Watu wengi hawapati habari kwenye magazeti kuhusu kazi ambazo zimetangazwa, au kazi zinazohitaji watu fulani. Watu tunaowatetea ni akina mama, wale wanaoishi na ulemavu na vijana. Wengi walilalamika sana na kusema ya kwamba hawapati taarifa ya kutosha. Tuliafikiana ya kwamba ni lazima tupitishe Ripoti hii. Kama Wabunge, ni muhimu tujielimishe kuhusu mambo kama haya yanayoendelea nchini Kenya, na ni lazima tutafute suluhisho. Namuunga mkono Mheshimiwa kutoka eneo Bunge la Kiminini. Amesema ya kwamba tuanze na sisi wenyewe kama Wabunge na sehemu zetu. Katika ofisi zetu, tumeandika watu kwa njia gani? Je, tumefuata sheria ambayo imewekwa katika Katiba yetu? Tuna Katiba na sheria kuhusu mambo ya ugavi wa nafasi za kazi nchini Kenya. Kwa hivyo, tumeileta Ripoti hii ili tujielimishe na tuanze na ofisi zetu. Kuna muda tuliuliza Wizara mbalimbali maswali mengi, na wakasema ya kwamba hakuna structure ya kutosha kuhakikisha taarifa zinafika mashinani zaidi ya kutumia magazeti. Tunajua bayana kwamba kuna watu ambao hawawezi hata kununua magazeti, na wengine wao hawana redio au namna yeyote ya kupata taarifa hizi. Hata ofisi ya Mbunge kule mashinani inaweza kupitisha habari hizi. Ningependa kuwaeleza Wabunge wanaonisikia kwa sasa ya kwamba ofisi zao zinaweza pia kuwa structure ya kutuma taarifa hizi. Kama viongozi, ni lazima tuonyeshe ya kwamba tunajali na tungependa watu mashinani wapate taarifa za nafasi za kazi katika wizara mbalimbali. Tunahitajika kuwa tayari kusikiliza kinachoendelea. Kama wawakilishi wa wananchi, ni lazima tuangalie na tuwawakilishe ili wapate taarifa. Kuna ofisi mbalimbali, na sio ya Wabunge tu peke yao. Kuna pia ofisi za County"
}