GET /api/v0.1/hansard/entries/1494330/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1494330,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1494330/?format=api",
    "text_counter": 47,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chimera",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika. Langu ni ombi la Kauli kuhusu uendeshaji wa kampuni ya Base Iron Limited au Base Titanium Limited katika mradi wa Madini ya Kwale Mineral Sands eneo la Msambweni, Kaunti ya Kwale. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni ya Kudumu ya Bunge Nambari 53(1), kuomba kauli kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Mazingira na Mali Asili kuhusu uendeshaji wa Base Iron Limited katika Mradi ya madini ya Kwale Mineral Sands uliopo Maumba, Eneo Bunge la Msambweni, Kaunti ya Kwale. Katika taarifa hiyo, Kamati inapaswa- (1) Kutoa nakala za awali za mkataba wa ununuzi wa Mradi wa Kwale Mineral Sands ulionunuliwa na Base Iron Limited mnamo Agosti, 2010, kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya titanium, pamoja na mikataba mingine yoyote ya ziada iliyofuata, inayohusiana na mradi huo. (2) Kueleza jumla ya fedha ambazo kampuni ya Base Titanium Limited imetowa hadi sasa kwa jamii inayohusika kwa mujibu wa kifungu cha 183 cha Sheria ya Madini ya mwaka 2016 kwa shughuli za Uwajibikaji kwa Jamii na kueleza iwapo kuna kiasi chochote cha fedha ambacho hakijatolewa kufikia sasa. (3) Kufichua maelezo ya mkataba wa maendeleo ya jamii kati ya Base Iron Limited na jamii ya eneo la Maumba, Msambweni, pamoja na kutoa taarifa ya hali ya utekelezaji wa mkataba huo na orodha ya miradi yote iliyotekelezwa na Base Titanium Limited kulingana na mkataba. Asante."
}