GET /api/v0.1/hansard/entries/1494357/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1494357,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1494357/?format=api",
"text_counter": 74,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kutoa mchango wangu kwa taarifa zilizoitishwa. Kwanza, ningependa kuchangia taarifa ya dadangu, Sen. Essie Okenyuri, kuhusu kutekwa nyara kunakoendelea. Ningependa kuzungumza na sisi viongozi na wananchi kwa jumla. Pindi mwananchi anapopotea, tusiwe na haraka ya kushuku kwamba ni Serikali imemchukua mtu kama yule kwenda kumfanyia labda mambo mabaya. Dhana ile inafanya wahusika wanaopaswa kufanya upelelezi wa kule aliyepelekwa yule aliyetekwa nyara kuwa ngumu kwa sababu tayari tumekwisha kunyoosha kidole cha lawama dhidi ya taasisi fulani."
}