GET /api/v0.1/hansard/entries/1494369/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1494369,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1494369/?format=api",
    "text_counter": 86,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "habari tuliona viongozi shupavu wa Seneti wakitetea kaunti ili fedha siziwe chini ya Kshs400 bilioni. Haiwezekani kuwalisha mamba na baadaye watule sisi. Haiwezekani tukeshe kila kuchao tukitetea wananchi wa kaunti zetu ili wapate pesa ilhali kuna viongozi ambao wana dhana kwamba sisi ni kama wanaosukuma rukwama kwa niaba ya watu wetu. Hatutakubali. Sen. Dullo amesema kwamba sekta ya afya imedorora. Wengine hapa wametuambia kwamba sekta za kilimo na elimu zimedorora, ilihali tukiita viongozi hao katika kamati zetu hawaji. Wanajipiga vifua na kubwata maneno yasiyoeleweka. Wakati umefika tuonane jicho kwa jicho. Kule mashinani, tunasema mundu khu mundu ."
}