GET /api/v0.1/hansard/entries/1494801/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1494801,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1494801/?format=api",
"text_counter": 34,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii angalau kutaja machache kuhusu mchecheto mzima wa mawaziri kukosa kuja hapa kujieleza kwa mapana na marefu. Bibilia inasema kwamba, Yesu alipokuwa anatembea na wafuasi wake, walimuona mwamamke mmoja wakamuita mzinzi na wakataka kumpiga mawe. Yesu kwa busara wake akawauliza ni nani miongoni mwao hana dhambi? Akawaambia yule asiye na dhambi atupe jiwe wa kwanza. Wengi walifyata midomo, wakaweka mikia katikati ya miguu na hatimaye wakamuacha binti huyo aliyekuwa anafanya biashara zake. Mhe. Naibu Spika, hakuna mtu duniani humu hana dosari ama makosa. Kuteleza sio kuanguka. Jumba la Seneti lina haki kikatiba kuwasikiza na wao kutupa majibu kuhusu changamoto zinazowakumba wakenya. Ni dhahiri shahiri kwamba mfumo wa afya una changamoto. Tumeona viongozi wa madaktari wakitoa ilani. Hayo yote tunakubali. Tunachotarajia ni kwamba Waziri wa Afya na yule mwenzake waje kwa Jumba la Seneti tujadili kwa pamoja na tutafute njia mbadala za kutatua changamoto hizi. Waziri wa Afya na mwenzake wako na nafasi ya kujieleza kwa sababu ni wataalamu wa mda mrefu. Wanaweza kutuma arafa ama watueleze siku ambayo watakuwa tayari wiki ijayo ili kazi tulionayo Seneti iweze kusonga kwa kasi. Sitaki kuwa yule mfuasi wa kutupa mawe katika kundi la wale wakristo waliotaka uponyaji. Naomba Seneti iwape The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}