GET /api/v0.1/hansard/entries/1494804/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1494804,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1494804/?format=api",
    "text_counter": 37,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika. Nina huzuni nyingi kwa sababu tuliposema Mawaziri watakuja hapa siku ya jumatano, tulikuwa na maono ya kusaidia mwananchi mashinani. Sisi kama Maseneta huwa tunatetea ugatuzi. Mawaziri wanafanya kazi mashinani ndio wananchi waweze kufaidia. Ninahuzunika kama Maseneta wataleta mambo ya ukoo na kuwatetea. Kuna Mawaziri tuliwatimua na tukaleta wengine wapya ambao wamekuja na ujuzi wa kufanya kazi. Wakati mtu ameteuliwa, anafaa kuanza kazi siku hiyo kama vile Yesu alipokuwa anateua wanafunzi wake na wanaanza kufanya kazi siku hiyo. Tuko na mfano wa Naibu Rais, Mhe. Kindiki Kithure, alivyoteuliwa. Yeye alianza kazi mara moja. Nimeshangaa kuona Seneta mwenzangu akimtetea mtu kwa sababu ni wa kabila lake. Tutauwa ugatuzi tukifanya hivi."
}