GET /api/v0.1/hansard/entries/1494849/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1494849,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1494849/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante Bw. Naibu Spika. Ni jambo la kusikitisha kuona kila kuchao, tukiwaita Mawaziri ambao wanatakikana kuja kuwajulisha wananchi wa Kenya na kujibu maswali ambayo yana umuhimu katika taifa la Kenya, hususan, upande wa afya, kunakuwa na upotevu wa kuja katika Bunge la Seneti kueleza Wakenya ni shida gani iliyoko. Mara nyingi, kumekuwa na vifo vya wagonjwa na ukosefu wa insurance wanaosema wananchi wanapata, ila wakifika hospitali wanajereshwa. Ni muhimu ikiwa Mawaziri hao wanaweza kujitokeza na kujibu haya maswali. Bw, Naibu Spika, la mwisho ni kwamba, itakuwa aibu na kusikitisha, ikiwa Waziri ameitwa kuja kujibu maswali katika Seneti na akose kuja. Huu ni ukiukaji wa sheria na Bunge hili linaweza kuchukua hatua ya kuwapatia summons kama zile za kortini ili afike hapa na akikosa kuja tena anaweza kupigwa faini. Bunge hili lina uwezo wa kuwapiga faini. Kuna umuhimu wetu tupeleke message ngumu ama ya uzito zaidi ili hawa watii agizo la hii Bunge la Seneti. Asante."
}