GET /api/v0.1/hansard/entries/1494851/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1494851,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1494851/?format=api",
    "text_counter": 84,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika. Ningependa kukemea sana kwa sababu saa hii, hasa katika Kaunti ya Kwale, nilikuwa nimejiandaa siku ya leo kumwuliza maswali Waziri wa Afya. Kuna wangonjwa wengi ambao wako katika Referral Hospital ya Msambweni wiki iliyopita. Nilienda nikashuhudia wagonjwa wakirudishwa kwa sababu ya hii mambo ya SHA. Sisi kama Wakenya tutakuwa huru ama tutajivunia afya lini? Hata waheshimiwa wenzangu leo walikuwa wamejiandaa kwa sababu katika kaunti zetu 47, shida kubwa saa hii ni hiyo insurance ya SHA. Nakemea sana. Ikiwa Waziri alijua yeye ni mgonjwa kutoka Jumatatu au Jumanne angetuma ujumbe mapema lakini ujumbe umekuja tu jana ama leo, ilhali watu wamejiandaa kuuliza maswali kupata mwafaka, kwa nini hii SHA inaleta shida katika kaunti zetu. Mhe. Naibu Spika, kama Seneta wa Kwale County nakemea sana. Siku nyingine huyo Waziri anafaa aje personally, na kama hawezi atuambie mapema “Siku fulani nitakuja”. Nakemea sana huyu Waziri. Anafaa arekebishe hii tabia. Hafai kutuma barua dakika ya mwisho halafu kesho tunamwona katika runinga akiwa Samburu. Hiy ni tabia mbaya sana na anapaswa akome. Watu wa Kwale County wanasema wanataka hii SHA ifanye kazi kwa haraka sana. Asante."
}