GET /api/v0.1/hansard/entries/1494947/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1494947,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1494947/?format=api",
    "text_counter": 73,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chimera",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa fursa hii. Naunga mkono Mswada huu. Kama kuna Mswada katika muda ambao nimekuwa katika Bunge hili ambao ni muhimu na unafaa kupewa kipaumbele ni huu ambao umeletwa hapa na Naibu Spika, Sen. Kathuri, kutoka Kaunti ya Meru. Ni jambo la kushangaza kwamba mabunge ya kaunti ambayo kisheria yanafaa kuwa mstari wa mbele kuhakiki magavana ama utendakazi wa serikali za kaunti yanakosa fedha. Tunayanyima mabunge ya kaunti fedha za kuendesha shughuli na biashara zao ilhali pesa hizo wanapewa magavana. Kwa kweli, ugatuzi uko katika hatari kubwa kwa kuwa kuna ubadhirifu wa fedha katika kaunti zetu kwa sababu mabunge ya kaunti. Hali hiyo inafanya wao kutoweza kufanya kazi yao. Tukiwapa Wawakilishi wa Wadi pesa, wataweza kufanya mikutano na kuhakikisha kwamba iwapo gavana au waziri wa kaunti hafanyi kazi yake anaitwa na kukosolewa ili kazi ifanywe sawa sawa. Wawakilishi wa Kaunti vile vile wana majukumu mengi. Lazima makatibu wa mabunge ya kaunti wanyenyekee kwa magavana na Mawaziri wa Fedha katika kaunti. Hali hiyo inafanya tunapoteza maana yote ya ugatuzi. Nampongeza Naibu Spika. Yeye mwenyewe aliona kwamba ipo haja ya kuhakikisha kwamba mabunge yetu ya kaunti yanawezeshwa ili waweze kufanya"
}