GET /api/v0.1/hansard/entries/1494955/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1494955,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1494955/?format=api",
"text_counter": 81,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika, ukiangalia kaunti yangu ya Kwale, kumekuwa na kelele na hatihati kuhusu hali ya utendakazi hususan katika Idara ya Afya. Mimi kama Mwanakamati wa Kamati ya Afya, nilikuwa na mkutano na MCAs wa Kamati ya Afya ya Bunge la Kaunti ya Kwale. Walinieleza kuwa tatizo kubwa ambalo linawasibu ni kwamba hawana hata fedha za kufanya kikao na waziri wao. Hawawezi kufanya mkutano na kutathmini hali ya afya katika kaunti hiyo. Hiyo ndio taswira katika kaunti nyingi. Si vizuri kiongozi kukosa sauti kwa sababu hana fedha. Nakuunga mkono. Kama kuna Seneta ambaye anafahamu kazi yake basi ni wewe kupitia Mswada huu. Nina imani kwamba Bunge hili limeona umuhimu wa kuhakikisha kwamba tunaunga mkono Mswada huu. Naomba sote tuunge mkono na kuupitisha haraka iwezekanavyo ili uwe sheria. Hiyo itawawezesha MCAs kufanya kazi yao pasipo kunyenyekea kwa magavana. Pesa zinapotolewa na Wizara ya Fedha ziende moja kwa moja kwa Makatibu wa Kaunti. Bw. Naibu Spika, nampongeza Sen. Osotsi na pia Kiongozi wa Wengi kwa kauli yao. Kuna maafisa ambao wamezoea kuleta nyokonyoko kwamba fedha haziwezi kuwafikia bila kuweka asimilia yao. Nafikiri hiyo si sawa kisheria. Ipo haja ya Sen. Osotsi kuleta marekebisho ili kuhakikisha kwamba fedha zikitoka katika Wiraza ya Fedha zinakwenda moja kwa moja kwa mabunge ya kaunti bila vikwazo vyovyote ili tuwape fursa MCAs kufanya kazi yao. Bw. Naibu Spika, kwa hayo mengi au machache, naunga mkono Mswada huu. Asante."
}