GET /api/v0.1/hansard/entries/1494978/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1494978,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1494978/?format=api",
"text_counter": 104,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii ili kuchangia Mswada wa Marekebisho wa Sheria ya Fedha 2023. Najiunga na maseneta wenzagu kukupongeza kwa Mswada huu ambao umekuja kujaribu kuwapa uhuru baraza za kaunti zetu ambazo ziko kwenye minyororo ya magavana wa kaunti zote 47. Nachukua fursa hii pia kutoa rambirambi zangu kwa mwendazake, Bw. Peter Oloo Aringo ambaye alileta Mswada wa kuidhibiti Bunge yani Parliamentary Service Commission (PSC) kwa mara ya kwanza. Alikuwa pia mwenyekiti wa kwanza wa Tume ya Bunge hili. Tume hii imeweza kuipa Bunge ule uhuru ambao hivi sasa kama Maseneta na Wabunge tunafurahia. Mswada huu unajaribu kuipa fursa Bunge za Kaunti kudhibiti na kupata hazina zao kivyao. Kwa sasa, fedha za Mabunge ya kaunti zinapitia kwenye Executive; yani hazina kuu ya kaunti na mwenye kusema pale ni gavana na waziri wa fedha. Mswada huu utawapa fursa Wabunge wa Bunge zetu za ugatuzi kuhakikisha wanafanya mambo yao kwa uhuru. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}