GET /api/v0.1/hansard/entries/1494979/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1494979,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1494979/?format=api",
    "text_counter": 105,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Mara nyingi wanapotaka kusafiri ni lazima wasubiri pesa zitoke kwenye hazina kuu. Wakitaki pia kufanya miradi yao vile vile ni lazima wasubiri pesa. Hili linachangia pakubwa mara nyingi wao kufungia macho zile dhambi zinazofanywa na Executive katika kaunti hizi. Malamiko mengi katika kaunti ni kuwa Bunge hizo hazifanyi kazi kikamilifu. Hili limesababishwa na ule uoga waliyonao kwamba iwapo wataweza kufanya kazi yao kikamilifu, basi magavana na wengine wengi watakuwa katika shida kubwa ya utekelezaji wa miradi ambayo inafanyika katika kaunti hizo. Jambo lingine nilikuwa nikitaka kugusia ni kuwa kwa sasa, ijapokuwa kuna uwiano, yani mediation unaoendelea kati ya Bunge hili na Bunge la Kitaifa kwa masuala ya ugavi wa fedha, kaunti zetu kwa muda wa miezi minne hazijapata fedha. Tumeona magavana wengi ‘wakipiga kelele na kulia’, kwa sababu mapato ambayo wanaokota katika kaunti zao hayawezi kulipa mishahara, kutekeleza huduma wala kununua madawa katika zahanati na hospitali. Iko haja ya kuiambia Serikali itumie kipengee cha sheria kinachosema kwamba wanaweza kupeleka asilimia 50 ya pesa walizopeleka mwaka jana. Kwa mfano, mwaka jana walipeleka shilingi bilioni 355 kwa kaunti zetu badala ya shilingi ya shilingi bilioni 385. Ukizingatia asilimi mia 50, basi wapeleke kiwango cha chini shilingi bilioni 150 ili kaunti zetu zisilemae kwa sababu ya ukosefu wa fedha za kufanya ile miradi ambayo imekusudiwa kufanyika. Bw. Naibu Spika, la mwisho ni, ijapokuwa tunajaribu kuzisaidia mabunge yetu ya kaunti ili yaweze kuwa na uhuru, mara nyingi, uhuru unatokana na wabunge wa kaunti zetu. Ikiwa watajiweka rahisi na saa zote kufuata vile ambavyo gavana ama mawaziri wanafanya katika kaunti, kazi ya uangalizi itakuwa ni shida sana katika kaunti zetu. Mara nyingi, unyonge uko kwa Wabunge wa kaunti. Sio kwamba sheria haiwalindi. Lakini tukiangalia, kazi kubwa wanayofanya kama vile kupitsha bajeti, hawawezi kulazimishwa kupitisha bajeti katika mabunge yao. Lakini mara nyingi huwa wanautepetevu na ukosefu wa uhuru ambao unawafanya wao kukubali yale ambayo yanafanyaika bila kutoa nafasi ya kuhakikisha ya kwamba wanaangalia maslahi ya umma na wananchi katika kaunti zao. Mhe. Naibu Spika, naunga mkono Mswada huu."
}