GET /api/v0.1/hansard/entries/1495456/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1495456,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1495456/?format=api",
"text_counter": 340,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Ahsante, Mhe. Spika. Ni vile sisi ni wawakilishi wa wananchi na wakituona tuko hapa leo lakini hatujauliza maswali yanayowahusu, tukirudi katika maeneo bunge yetu, tutakuwa na shida. Mwanzo, ningependa kumpongeza Waziri kwa vile yeye ni mungwana sana. Tunapoenda ofisini mwake, huwa tunapokelewa vizuri. Ninataka Waziri ajue kuwa Lamu Mashariki ndio eneo bunge pekee Kenya ambalo halina hata inchi moja ya barabara ya lami. Eneo Bunge la Lamu Mashariki lina barabara tatu. Mojawapo ni barabara ya Mtangawanda- Kizingitini ambayo mnaijua. Ninaomba mtueleze mikakati ya ujenzi wa barabara hiyo imefikia wapi angalau tuwe na barabara ya lami. Barabara ya pili ni ya Hindi-Kiunga ambayo ni kilomita kama 120. Barabara hiyo haipitiki wakati huu kwa sababu ya wahalifu wanaoweka Improvised Explosive Devices (IEDs ) kwenye barabara hiyo. Barabara hiyo imefungwa kabisa kwa sasa. Wadi mbili katika Lamu Mashariki hazipitiki. Lazima upitie baharini kwenye boat na wakati mwingine, bahari ni shida sana. Kwa hivyo, ninamuomba Waziri afikirie Lamu Mashariki na kutengeneza hata sehemu ndogo tu ya barabara ya lami ili eneo bunge hilo lifunguke. Ninasikia pesa imepewa Mchina. Kama security ni shida, the Kenya Defence Forces (KDF ) wako tayari, wanafanya kazi vizuri na wanapeana security . Kwa hivyo, wafanyikazi wa Ministry wapewe KDF waeneze usalama ili barabara ifunguke."
}