GET /api/v0.1/hansard/entries/1495468/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1495468,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1495468/?format=api",
    "text_counter": 352,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika. Ningependa kumpongeza Waziri na kumuuliza swali kuhusu Kivukio cha Feri cha Mtongwe ambacho kilisitisha kuwapa huduma wakaazi wa Likoni. Hivi sasa, tukiangalia Kivuko cha Likoni, kumekuwa na msongamano mkubwa sana na hatari kubwa sana za ajali. Tutakuwa na michezo ya EastAfrican Legislative Assembly (EALA) hivi karibuni katika Mombasa. Ninamuuliza Waziri, ni mikakati gani ambayo tutaweka ili tupunguze ule msongamano? Hii ni kwa sababu Kivukio cha Feri cha Mtongwe kilikuwa kinapunguza msongamano wa abiria. Kile kivukio cha kuelea tunachokiita kwa lugha ya Kiingereza “ floating bridge ” pia kilikuwa kinasaidia. Hivyo vyote vimeondolewa na hivi sasa, kumekuwa na msongamano mbaya sana unaoleta athari za ajali nyingi. Swali la mwisho ni kuhusu Barabara ya Dongo Kundu. Tunaishukuru Serikali kwa kung’ang’ana kutengeneza barabara hiyo. Imebaki hatua kidogo sana ili ifunguliwe rasmi na Mhe. Rais (Dkt.) William Ruto. Lakini kuna hatari katika barabara hiyo kwa sababu ya mwanya ulioachwa wazi. Juzi tumempoteza kijana ambaye alitumbukia baharini na kupoteza maisha yake kwa sababu barabara hiyo iko juu na chini ni bahari. Tunamuomba Waziri aangalie swala hilo ili barabara hiyo imalizwe, Rais aifungue rasmi, na hatari kwa wale wanaoitumia barabara hiyo izingatiwe. Ahsante sana, Mhe. Waziri."
}