GET /api/v0.1/hansard/entries/14955/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 14955,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/14955/?format=api",
"text_counter": 345,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Ninasimama kwa masikitiko makubwa sana nikisema kwamba sisi kama taifa, tuliumia wakati wa Ukoloni. Tuliteswa kabisa. Na ni kwa sababu ya dhuluma kama hizi ndiposa wananchi wakaamua kwamba ni lazima wamng’oe mkoloni ili haki zao zilindwe. Baada ya mababu wetu kupigania nchi hii ili ubaguzi wa haki za Wakenya usimamishwe, inaonekana kwamba tunaishi katika himaya ya kikoloni kupitia watu wetu ambao wanastahili kulinda na kuzingatia maslahi ya Wakenya. Ukiangalia mambo ambayo yametajwa katika Ripoti hii ambayo imeletwa na Kamati ya Bunge, utaona kwamba sheria kuhusu wafanyikazi katika taifa letu la Kenya imo kwenye kitabu tu na haijaweza kudhihirishwa kulinda haki za Wakenya."
}