GET /api/v0.1/hansard/entries/14956/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 14956,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/14956/?format=api",
    "text_counter": 346,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Ukiangalia, utapata kuna mwananchi wa taifa hili ambaye amezaliwa na mzee na mama wa taifa hili. Juu yake, kuna mtu ambaye amesomeshwa na taifa hili, na yuko kwenye madaraka na anastahili kulinda haki ya yule Mkenya. Lakini utasikia kwamba mtu huyo amefanya kazi miaka 14 na bado rekodi za uajiri wake zinaonyesha kwamba yeye ni mfanyikazi wa kibarua. Ukiteremka, utapata kuna miaka mingine 10, saba, tatu na kadhalika. Bw. Naibu Spika wa Muda, mateso bila chuki yanaenezwa kwa mwananchi wa taifa hili ambaye anachagua Wabunge kama sisi. Kuna sheria za kikazi na kuna Serikali ambayo inafaa kumlinda ambayo iko na Rais na Makamu wa Rais, lakini mtu huyo anaachishwa kazi. Mbunge wa sehemu hiyo anatatizika na kuleta Hoja kama hii ilhali kuna sheria ambayo inafaa kulinda haki ya Mkenya huyu kabla jambo hili halijafika hapa. Ripoti imesema kwamba hata huenda pesa hizi hazitalipwa kwa haraka kwa sababu kutakuwa na visingizio eti mambo haya yako mbele ya korti na ni lazima korti itoe uamuzi huku yule mwananchi wa kawaida ambaye amechagua Serikali na kuiweka kwenye madaraka anateseka."
}