GET /api/v0.1/hansard/entries/14957/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 14957,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/14957/?format=api",
    "text_counter": 347,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Hakuna haki, ukweli na usawa katika mambo ambayo yanatendeka katika nchi yetu. Pesa ambazo watu 250 wanaitisha hapa ni Kshs9.5 milioni. Kwa uwazi na udhahiri, wale wezi hodari katika taifa letu ambao wanaiba pesa kidogo, wanaiba Kshs10 milioni. Hapa, tunauliza Kshs9.5 milioni kwa wananchi 250. Leo, tuna uhakika na uwazi kwamba wezi wale wa katikati ni wale ambao wanatoroka na Kshs5 milioni halafu wale wa juu hawajulikani. Wakenya hawa wanadai haki yao ilhali yule Karani wa Mji ambaye ameelimishwa na taifa hili na kuwekwa kwenye madaraka, mshahara wake hauchelewi. Bw. Naibu Spika wa Muda, sijui kama tumepata Uhuru au tunataka kurudi kupigania Uhuru. Kama mwananchi wa kawaida hana haki ya kutumikiwa, basi Uhuru uko kwa walio juu. Mabeparri wako wakubwa lakini mtu wa chini hana haki ya kujitetea."
}