GET /api/v0.1/hansard/entries/14958/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 14958,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/14958/?format=api",
"text_counter": 348,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Hawa wananchi wa Juja ni chanzo tu cha matatizo yanayowakumba Wakenya. Ukienda kwa kila mji, utaona kwamba wananchi wanaajiriwa kwa kazi ya kibarua. Hata kampuni za kibinafsi zimepenya katika Wizara na kuwajiri watu wao kusimamia dhuluma kwa Wakenya. Mwananchi wa kawaida akienda kudai haki yake kwa shirika la kibinafsi, anaambiwa aende ofisi ya wafanyikazi. Akienda ofisi ya wafanyikazi, anakuta yule mtu ambaye amewekwa huko anapata mshahara na anarudia kwa mlango na hawezi kupata haki yake. Ukiingia katika kila sehemu ya uakilishi Bunge, utaona kuwa wananchi wako na matatizo hayo."
}