GET /api/v0.1/hansard/entries/14960/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 14960,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/14960/?format=api",
    "text_counter": 350,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Nimekaa hapa kutoka asubuhi ili nizungumze kuhusu jambo hili na wananchi taifa nzima wanisikie. Kwa hivyo, ningependa kuona matokeo. Hatutakubali mambo haya kamwe. Kama ni kulipwa, walipwe na wale wengine ambao wanadai, vile vile, walipwe. Waziri wa Kazi na Mawaziri wengine ambao wanahusika wajue kwamba viti ambavyo wanakalia si vya maridadi tu. Sio viti vya bendera, gari na ofisi tu, ila mwananchi wa Kenya anataka kupata huduma kutoka kwa Wizara hizo. Moja ya utumishi huu ni kuondoa dhuluma. Bw. Naibu Spika wa Muda, Ripoti hii inaendelea kusema kwamba Karani wa Mji apelekwe kortini na kushtakiwa. Ikiwa mtu ambaye amesoma na anaelewa sheria anangojea Kamati ya Bunge kumkaba koo na kumwambia ni lazima aende kortini kwa sababu amefanya dhambi, basi sijui tutaenda wapi. Ni lazima watu hawa wajue kwamba kazi yao si kupata mshahara tu. Ni lazima watumikie taifa hili na waimudu nchi ili iweze kutoa watoto ambao wanaelewa sheria zaidi ili wanapopata madaraka, waweze kutumikia taifa hili vizuri. Kuna kisingizio kwamba watu ambao wameajiriwa ni jamii ya mtu mmoja. Hao watu wakiajiriwa, walikuwa na kazi zingine halafu wakapewa kazi zingine au ni wale Wakenya ambao wanaambiwa: “Wewe, hauna kazi, ingia kazi”. Itakuaje kama mtu ambaye yuko ofisini, nyuma yake hawezi kufanya kazi na mtu ambaye hawana ukoo naye, ili asihusishwe na dhana kuwa ameajiri watu wake? Walioajiriwa hawawezi kufutwa kwa kisingizio kwamba wao wanauhusiano na wakubwa ambao wanawaongoza. Hao ni Wakenya na wanafaa kupewa kazi. Uchunguzi hapa umefanywa na umeonyesha kwamba sheria za wafanyikazi hazikufuatwa. Ni jukumu la Waziri kuona kwamba mambo hayo yamefanyika. Ninamshukuru mhe. Kabogo kwa kuleta Hoja hii Bungeni ili iwe kielelezo katika miji mingine na siyo tu katika Wizara ya Serikali za Mitaa lakini kwa taifa nzima. Kwa hayo machache, ninaunga mkono. Ninaishukuru Kamati iliyoandika Ripoti hii."
}