GET /api/v0.1/hansard/entries/1496881/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1496881,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1496881/?format=api",
"text_counter": 103,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada wa Uchangishaji Fedha wa 2024. Kwanza nampongeza Kiongozi wa Wengi kwa kuuleta Mswada huu katika Seneti. Ikumbukwe kwamba hapo nyuma kabla ya mzozo tuliokuwa nao katikati ya mwaka huu, masuala ya harambee yalikuwa kama mashindano. Wenzetu walikuwa wanaenda kwa harambee na magunia ya fedha. Wananchi wanaambiwa wahesabu na wanahesabu mpaka inafika shilingi milioni 20 hadi ile hesabu inapotea. Ukifanya utafiti wa tarakimu ambazo mchangishaji yule amewasilisha mapato yake ya kodi kwa Kenya Revenue Authority (KRA) mwisho wa mwaka, hana mapato ya shilinhi milioni 20. Hawezi kuonyesha kodi aliyolipa kutokana na mshahara wa kazi ama biashara iliyompatia hizo shilingi milioni 20. Kwa hivyo, harambee zilikuwa zimefika kiwango ambacho wengi wanazitumia vibaya. Ilikuwa ni mambo ya mashindano. Hatukatai hayo kwani hata dini yetu ya kiislamu inakubali watu washindane katika mambo ya kheri. Lakini ilikuwa imefikia kiwango ambacho inakejeli hata wananchi waliochangishiwa pesa zile. Katika muktadha huo ndio Kiongozi wa Wengi amekuja na Mswada huu wa ili kurekebisha na kutia nguvu masuala ya uchangishaji pesa. Bw. Spika, harambee zimesaidia nchi hii pakubwa kutoka wakati Hayati Mzee Jomo Kenyatta alipoanzisha mfumo huu wa maendeleo. Tumeona shule na hospitali zimejengwa na mambo mengi yamefanyika katika mfumo huu wa harambee. Kwa hiyo Mswada huu haunuwii kuua harambee, bali malengo yake ni kuleta usawa na uwazi katika masuala ya harambee. Pia kudhibiti mwenendo wa maafisa wa umma katika masuala ya harambee. Mara nyingi tumeona watumishi wa umma kama sisi wakialikwa kama wageni wa heshima katika harambee fulani, basi watachangisha nusu--- Kuna mkutano wa Nothern Frontier Province (NFP)---"
}