GET /api/v0.1/hansard/entries/1496885/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1496885,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1496885/?format=api",
    "text_counter": 107,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Mswada huu unalenga kuleta mfumo wa harambee ambao utasaidia taifa na kaunti zetu katika masuala ya uchangishaji pesa kusaidia miradi mbalimbali ambayo wananchi wanachangisha pesa. Pili, iwapo Mswada huu utakuwa sheria, basi sheria hii itaondoa ama repeal the Public Collections Act, Cap 106 ya sheria zetu za Kenya. Sheria hiyo hailingani na mfumo wa sasa wa ugatuzi katika nchi yetu. Tukiangalia vipengele tofauti vya sheria hii, inaangalia pande zote mbili za Serikali. Kuna harambee za kitaifa ambazo lazima ziandikishwe kupitia kwa Waziri wa Serikali Kuu na kuna harambee za kaunti ambazo zitaandikishwa kupitia kwa county executive wa kaunti husika. Zote hizi zinatakikana kuandikishwa katika sehemu zile. Vilevile sheria hii inatoa fursa ya kutofautisha uchangishaji kwa umma na wa kibinafsi. Kwa mfano, nikiwa nataka kufanya harambee naweza kualika watu fulani pekee yake. Kwa mfano, naweza mualika, Sen. Cherarkey, Sen. Tabitha Mutinda na wengineo ambayo haitakuwa harambee ya wazi, yaani public fundraiser. Mswada huu unasema kwamba sio lazima kuandikisha hizi harambee za kibinafsi. Hii inamaanisha zitakuwa huru. Sheria hii inatunyima nafasi ya kuhusika katika masuala ya harambee. Kwa hivyo, Wabunge na maafisa wa umma wengine watakuwa hawaruhusiwi kushiriki katika harambee. Sen. Cheruiyot alipokuwa akiongoza Mswada huu alisema kuwa hata wale ambao wanania za kugombea viti miaka mitatu kabla ya uchaguzi hawatahusika na maswala yoyote ya harambee nchini. Vile vile, yule msimamizi wa harambee lazima atafute permit ili aweze kuendesha harambee. Wengi wanasema kuwa harambee inaleta vikwazo. Lakini ipo haja kwa sababu tumeona kwamba wengine walichangisha pesa kwa madhumuni fulani na baadaye hawakuweza kutekeleza yale madhumuni waliotarajia. Vile vile, kuna harambee nyingi gushi. Pesa zikisha ingia zinatumika kwa mambo ambayo haya kukusudiwa katika harambee ile. Bw. Spika, Mswada huu unatoa mwongozo kwa masuala ya harambee kwa undani zaidi. Ningeomba Maseneta wenzangu waweze kuisoma. La msingi ni kwamba hakuna harambee ambayo inapingwa na Mswada huu. Ule uwezo wa Wabunge na maafisa wa umma kuweza kuendesha harambee na kuenda kwenye harambee na mamilioni ya pesa ambazo hatujui zimepatikana vipi ndio inayopingwa kwenye Mswada huu. Sheria hii pia inatoa nafasi kwa Waziri kutengeneza sheria endelevu yaani"
}