GET /api/v0.1/hansard/entries/1496980/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1496980,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1496980/?format=api",
"text_counter": 202,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Mambo ambayo mimi nimeyapitia, na wengi wanaokaa katika Seneti, naweza kudhihirisha ya kwamba wanaoketi hapa wengi walipita na kusoma kwa sababu watu walikuja pamoja kwa harambee wakawachangia pesa. Kwa hivyo, ile njia iliyowapitisha kuwafanya walivyo siku ya leo, mimi naomba tusije tukaifunga. Kwa nini? Angalia mtu aliyefiwa kwa sababu ya kukosa matibabu. Mwili unafungiwa makafani kwa sababu familia haina pesa ya kuutoa. Labda mwendazake alikufa kwa sababu ya ukosefu wa matibabu. Kama tungelainisha maneno na kuhakikisha kuwa matibabu yanapatikana, pengine tungezuia vifo na hakuna mtu angeitishwa pesa."
}