GET /api/v0.1/hansard/entries/1496981/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1496981,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1496981/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Najua kuwa mnachangia sana kulipa karo za wanafunzi kwa kupeana bursary . Tumeongea sana kuhusu jambo hilo. Kuna Mswada unaonuia kufanya elimu kutoka kiwango cha chekechea hadi chuo kikuu bila malipo. Mswada huo ukiwa sheria, hakuna mtu atatuita kwenda kuchangisha pesa ya watoto kwenda shuleni. Kwa nini tusianze na kutengeneza sheria ambazo nimetaja? Kule kwetu, kuna msemo kuwa anayekula kwa kijiko huwa hajui kuchomeka kwa anayekula kwa mikono. Kama sisi tuna bima, hatuna matatizo na hatutaki kuchangiwa, tusisahau kwamba wanaoitisha msaada wana shida na wanafaa kusaidiwa. Bw. Spika wa Muda, kwa kumalizia, nilipokuwa nimeketi hapa, nilipata jumbe kadhaa za watu ambao wanaomba msaada kupitia harambee. Wote wanaoitisha msaada wana sababu za kutosha ili waweze kuokolewa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}