GET /api/v0.1/hansard/entries/1498238/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1498238,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498238/?format=api",
"text_counter": 398,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Jambo lingine ni kuwa juzi nimeona wakaazi wa Mombasa wakilalamika, wakisema wameletewa public participation wakati tayari ile tax ishaongezwa. Kuna mtu alisema walikuwa wanalipa ile licence Ksh26,000, na akiangalia kwa system, tayari imefika Ksh40,000 na bado public participation haijafanywa. Sio Mombasa tu! Hii inatendeka sehemu nyingi. Uchumi umekua mgumu sana. Kabla tufanye jambo lolote katika kaunti, ni bora tuhakikishe kwamba sheria inafuatwa. Inafaa public participation ifanywe kwanza ili tuone maoni ya wananchi ni yapi. Juzi, nimeona Chairperson wa Kamati ya Fedha na Mipango ya Kitaifa akizunguka Kenya nzima kuhusu maswala ya Finance Bill . Kwa hivyo, wafanye publicparticipation kwanza. Hii yote, imeletwa na utepetevu katika kaunti zetu, ambapo wanaleta taxes nyingi sana na wananchi wanaumia kule chini. Kwa mfano, kabla ya waiver, ile fine ilikuwa pesa ngapi? Pengine, mtu alifaa kulipa Ksh7,000 kwa mwaka. Kwa hivyo, usimpige fine ya Ksh21,000, ambayo ni mara tatu. Ongeza one per cent, something that is very reasonable . Sio kumfinya mwananchi, halafu sheria inamfinya zaidi ili aweze kulipa ile fine . Maanake hapa, tunaelezewa kuwa watoe sababu ya kumtolea mtu waiver . Wakenya wana matatizo mengi. Inaweza kuwa muda wa kulipa umefika, lakini mtu hajapata pesa za kulipa. Kwa hivyo, aongezewe fine kidogo ambayo ni reasonable. Katika Bunge hili, tunasema wapatiwe mwanya wa kukusanya zile fines bila waiver . Lakini fine huwa pesa nyingi zaidi ya ile pesa walikua wanafaa walipe. Kenya inahitaji ushuru ndio tujenge taifa. Lakini, sasa twende hatua baada ya hatua, tusimfinye mwananchi sana. Inafaa Wakenya waelewe kuwa bila kutoa ushuru, hatuwezi kulijenga taifa. Kwa hivyo, kama wewe ni mwanabiashara, toa ushuru mapema ndio ujenge taifa, na upate maendeleo kama ujenzi wa barabara na mashule. Lakini tukikwepa kulipa tax, tutaliregesha taifa nyuma. Kama nilivyosema pale mwanzo, hata ile Finance Bill inayozunguka isiwe ya kila mwaka. Mkenya apatiwe mwanya wa kupumzika. Ile Finance Bill iweze kutusukuma miaka miwili au mitatu. Baadaye, tukiona uchumi umekuwa sawa, tunaweza"
}