GET /api/v0.1/hansard/entries/149824/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 149824,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/149824/?format=api",
"text_counter": 543,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ni jambo la kufadhaisha mno kuona kuwa wale ambao wamepewa nafasi hizi za kuhudumia nchi yetu, hawana mwelekeo, habari na wengi hawajui kazi zao. Lakini si makosa yao maana walienda kwa wananchi kuomba kura. Walipopatiwa kura, lilikuwa ni jukumu la Serikali kuwapatia mafunzo. Kama wewe umeingia Bunge, umepatiwa kazi ya Waziri, swala nyeti la kuuliza ni: Je, hiyo kazi ambayo umepewa, unaiweza? Kama hauiwezi, Serikali imefanya nini kuhakikisha kuwa imekupatia mafunzo na maandalizi ya kutosha ya kukufanya uweze kuhudumu vilivyo katika kazi yako? Mara nyingi tunaona mtu ameingilia kazi ambayo amepewa lakini hana nyuma wala mbele. Ndio maana kila wakati unakuta Mawaziri wanazozana na Manaibu wao. Ni jambo la kufadhaisha kama vile juzi, Waziri alitoa hoja yake kuhusu michezo na Wasaidizi wake wakaanza kuzozana naye. Wote walikuwa hawana msingi. Kama wangekuwa wamepewa mafunzo ya kutosha ya nidhamu, maendeleo na kuendeleza Wizara yao, tokeo kama hilo halingetokea hapa Bungeni. Je, Mawaziri wote tulionao wanamshauri Rais? Je, tunawahitaji hawa Mawaziri wote? Wanahudumu jinsi inavyohitajika kulingana na mishahara wanayolipwa? Mara nyingi tunagundua kwamba hawahudumu vilivyo wala hawampatii Rais ushauri. Hii ni kwa sababu ni wengi mno. Vikao vyao vimekuwa kama mabaraza tunayokuwa nayo kule vijijini kwa sababu wote wanataka kuchangia ilhali haiwezekani. Hii ndiyo maana kila wakati mambo yetu yanaenda mrama. Tunaiomba Serikali ichukue muda wakati huu ili ichunguze makatibu wake wa kudumu. Je, makatibu wa kudumu ambao wanateuliwa wamechunguzwa kwa undani? Labda itafaa ikiwa majina yao yataletwa hapa Bungeni ili tuyachambue na tuweze kubainisha ikiwa mtu anaweza kufanya hiyo kazi. Je, tunapeana kazi kwa sababu, labda, mtu alitusaidia wakati wa uchaguzi? Huenda mtu anapewa kazi kwa sababu alimsaidia Rais akiwa katika harakati za uchaguzi. Wakati umefika nchi hii kusimamiwa kikamilifu na watu waliohitimu."
}