GET /api/v0.1/hansard/entries/1498272/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1498272,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498272/?format=api",
    "text_counter": 432,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi North, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Owen Baya",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Bwana Spika wa Muda. Ndugu yangu, Mhe Bady, anasema kwamba Wabunge watakapofika Mombasa, wasiende kuwalazimisha mabinti wao. Baadhi ya Wabunge wako na ndoa zao na kwa hivyo, hawawezi kuwanyemelea wasichana. Wanaenda Mombasa kushiriki kwenye michezo. Michezo hiyo itachezwa pale uwanjani mchana, na hamtakuwa na maneno mengine yanayowahusu wasichana. Sisi tutawapelekea pesa tu. Hawa Wabunge hawana haja, tamaa wala chochote kuhusiana na wasichana wa Mombasa. Hivyo basi, nataka kuwaambia wasichana wa Mombasa waje pale ili wapakulie wageni chakula na wafanye biashara zao. Yetu ni kuwaombea Mungu pekee. Ahsante."
}