GET /api/v0.1/hansard/entries/1498827/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1498827,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498827/?format=api",
"text_counter": 421,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Mhe. Spika, niko na tatizo lingine linalotokana na swala hili. Waziri, Lamu Mashariki ina wakulima wa simsim na hawatumii madawa yeyote. Lakini kuna shida kwa sababu majirani wetu wanatumia madawa ya kuua wadudu. Kwa hivyo, simsim zao zilizopelekwa kwenye soko za nje, zilirudishwa. Kutokana na hayo, zimeharibia sifa wakulima wote wa simsim. Ninavyoongea, simsim zimejaa kwenye soko za Lamu Mashiriki. Uko na mipango gani ya kuwasaidia wakulima hao ili mazao yao ya simsim yaweze kuuzwa? Wakulima wa Lamu Mashariki wako tayari mazao yao ya simsim yapimwe maana wao hawatumii madawa za kuua wadudu. Kama vile maziwa inapokuwa nyingi kupita kiwango cha soko, Serikali hufanya mpango wa kununua na kuhifadhi. Nasi kama wakulima wa simsim, tunawasihi mje na mpango wa kuwasaidia wakulima ili mazao yao yasiharibike na pia wafaidike."
}