GET /api/v0.1/hansard/entries/1498882/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1498882,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498882/?format=api",
"text_counter": 476,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Mhe. Naibu Spika, swali nililouliza halikujibiwa. Limepotea na ameambiwa aende kisha atarudi. Swali langu ni kuhusu simsim . Ningependa nilirejelee. Watu wangu walikuja kuniambia kwamba wako na shida. Kuna wakulima wa simsim Lamu Mashariki na wameniambia kwamba majirani wao wanatumia madawa na bidhaa zao zilirejeshwa. Hilo limefanya wao kupoteza soko. Simsim iko nyingi kule na haina soko. Je, mko na mipangilio ipi kusaidia hao wakulima wa Lamu Mashariki? Wao pia ni Wakenya. Ministry of Agriculture and Livestock Development inafanya kazi sehemu zingine, lakini Lamu Mashariki ni kama hakuna wakulima ilhali tuko nao. Tunazalisha c ashew nuts nyingi zaidi Kenya. Watu wa Kilifi wanasema kwamba wako na cashew nuts lakini miti yao ni mizee. Ukiangalia hesabu, korosho zetu ndizo zinazozalishwa kwa wingi zaidi. Nina uhakika hakuna chochote ambacho Wizara hii imefanya Lamu Mashariki. Au aniambie ni nini amefanya Lamu Mashariki. Ahsante."
}