GET /api/v0.1/hansard/entries/1498908/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1498908,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498908/?format=api",
"text_counter": 502,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Naibu Spika, niko kwa hoja ya nidhamu. Je, ni haki Waziri kusema ataenda kuuliza county government na tuna hakika wafugaji wa simsim kwetu Lamu Mashariki hawajawahi kusaidiwa na chochote na serikali hiyo? Wanajitegema wenyewe ilhali sehemu zingine wakulima wa maziwa, majani chai, kahawa, na muguka, wote wanapata fedha kutoka kwa Serikali ya kitaifa. Nilikuwa natarajia aniambie mikakati iliyopo na kama hana saa hii, aniambie atarudi Jumatano anielezee ana mikakati gani. Si vema kuniambia niende kwa serikali gatuzi niulize Gavana. Mimi si Seneta wala mwakilishi wa wadi!"
}