GET /api/v0.1/hansard/entries/1498942/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1498942,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498942/?format=api",
    "text_counter": 536,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Ningependa kumuuliza Waziri swali ambalo haswa limenileta hapa Bungeni leo. Hapa Bunge, tulipitisha kuwa factory ya korosho ifufuliwe na ianze kazi. Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji. Tulikuwa kule Pwani tukitegemea kuwa utafika kule ili utatue hiyo shida. Waziri, watu 4,000 walikuwa wanafanya kazi kwenye hivyo viwanda. Tuko na watu takriban 50,000 ambao wanategemea ukulima wa korosho. Licha ya usimamizi kupewa mtu binafsi, bado hatujaona manufaa yake katika Kaunti zote za Pwani. Nahisi uchungu nikiona Jumba hili likizungumzia jinsi kilimo cha kahawa na majani chai kinavyostawi. Pwani tumesahaulika sana. Na ndiyo maana tuliwahitaji sana wakati tulienda kutembelea ule mtambo ambao umechukuliwa na kampuni ya kibinafsi. Hatukuruhusiwa kuingia mle ndani. Mswada uliletwa hapa na Mheshimiwa Owen Baya na ukapitishwa kwamba kiwanda cha korosho kule Pwani kifufuliwe. Mpaka sasa, hatujaona matokeo. Ukulima wa nazi pia umedorora. Bandari ya Mombasa ni yetu lakini inaingiza nazi na korosho kutoka nchi za nje"
}