GET /api/v0.1/hansard/entries/1498944/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1498944,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498944/?format=api",
    "text_counter": 538,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "wakati wakulima wetu wanahangaika na kubobea kwenye umaskini ilhali miti ya korosho iko nchini. Ningependa Waziri anipe sikio. Najua hakuwa kwenye hiyo ofisi wakati huo, lakini ameweka mikakati gani kuhakikisha kuwa kiwanda cha korosho kinafufuliwa kama tulivyopitisha hapa Bungeni? Tunataka mmea wa maembe kuzinduliwa na kuinuka vizuri na nazi zetu kufufuliwa. Nahisi uchungu nikiwasikia wenzangu wakizungumzia bei ya macadamia kushuka wakati sisi wakulima wa korosho hatuonekani mahali. Nilitaka kumwuliza Waziri wa Elimu kabla hajaondoka kuhusu zile nafasi za kazi alizozitoa maana Kaunti ya Mombasa tulipewa nafasi tatu pekee kati ya 56,000 zilizokuwepo, ilhali tuko ndani ya broad-based Government . Tunataka tuone matunda ya Serikali hii pana ili tukisimama kwenye majukwaa yetu na kuwaeleza wananchi wetu yale mambo Rais amefanya, wataamini. Tunataka matendo. Rais amewawekea majukumu ya kumsaidia ili anapofika sehemu Fulani, atakuwa na mambo ambayo atasema amewafanyia wananchi. Lakini mkimwangusha kwa utendakazi wenu, atapata shida mashinani. Naomba mikorosho ifufuliwe katika Kaunti ya Pwani."
}