GET /api/v0.1/hansard/entries/1499347/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1499347,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499347/?format=api",
    "text_counter": 210,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda. Yangu ni ule utaratibu ambao unahitajika kwa wale ambao walikuwa wamejiandikisha katika ule mfumo uliopita wa NHIF na sasa na huu mfumo mpya. Tunafahamu kwamba hata sisi kama Wabunge tulikuwa tumechukua majukumu kupitia mfumo wetu ule mfuko wa National Government – Constituencies Development Fund (NG-CDF) kuandikisha baadhi ya wale ambao wanahitaji usaidizi. Walioandikishwa wakati ule walikuwa ni wale watu ambao hawajiwezi, wazee, wakongwe, na mayatima na hawana namna yoyote. Na katika huu utaratibu ulioko ni kwamba inabidii waweze kusafiri Kwenda vituoni na kujisajilisha upya. Ilikuwa ni ombi kwa Mwenye Kiti wa Kamati husika kama ataweza kufanya utaratibu wa kuwatembelea wale ambao hawajiwezi kuona ni vipi wataweza kuhamishwa. Wengi wao bado wako katika ule mfumo wa zamani, na kama wenzangu walivyotangulia wamesema, wakiwa na dharura na kwenda hospitalini, hawapati matibabu yoyote. Kuna utaratibu gani ambao wanaweza kufanya wa dharura ili wale ambao hawawezi kwenda kwa vile vituo waweze kusajiliwa ili waweze kunufaika na hili jambo?"
}