GET /api/v0.1/hansard/entries/1499447/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1499447,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499447/?format=api",
    "text_counter": 310,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia hii nafasi ili nami nichangie huu Mswada. Usimamizi wa mazingira na utaratibu ni muhimu sana katika kushugulikia maswala magumu ya mazingira. Ninachukua fursa hii kuunga mkono na kumpongeza dada yetu, Mhe. Irene Mayaka, kwa kuleta Mswada wa aina hii. Mhe. Spika wa Muda, katika kufuatilia jambo hili ni muhimu sana tuwe na utawala wa ushirikiano yani collaborative governance. Vile ambavyo imezungumuzwa jambo hili haliwezi kuonekana linashughulikiwa na watu fulani peke yao. Ni muhimu kaunti na Serikali kuu kuangalia jinsi litashughulikiwa. Mwisho zaidi, jambo hili linafaa kuwa na mapito ya kijumla ya mfumo, yani kwa lugha ya kiingereza systematic mapping reviews. Ni muhimu sana kuangalia miti hii inapandwa mahali gani na namna gani. Miti hii ya eucalyptus inaleta maadhara makubwa sana ikipandwa kando ya mito. Inakunywa maji sana na kukausha sehemu hizo. Kwa hivyo, ni lazima tutafute mbinu mbadala. Ndugu zetu wamesema katika Kaunti ya Kisii miti hii imelete shida kubwa. Walio pembezoni mwa mito, pendekezo langu ni kwamba wapande miti ambayo haitaleta madhara. Kwa sababu, kando na kunyonya maji yote, miti ya eucalyptus inadhoofisha nguvu ya …"
}