GET /api/v0.1/hansard/entries/1499456/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1499456,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499456/?format=api",
"text_counter": 319,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nimeridhia kwa kupewa msamiati huu na ndugu yangu Mhe. Tandaza. Yeye amebobea katika mambo haya. Walikuwa wakipanda miti kule Matuga Constituency. Yeye pamoja na Bi. Karuga walikuwa wakitoa miti ya mkalatuzi ili isipandwe na kudhoofisha hali ya udongo au mchanga. Zaidi ya hayo, jambo lolote la kimazingira ni la kutiliwa maanani. Ninataka kumpongeza Mhe. Irene Mayaka kwa kuleta Mswada huu. Ningependa kumwambia dadangu kwamba tutashikana na kumuunga mkono. Tumeona watu wengi sana hawatilii mambo ya mazingira maanani. Lakini, mazingira ndiyo yanayotupatia chakula. Leo tukiangalia nchi ya Burkina Faso, Raisi wao anasifika kwa sababu watu wake wanaishi bila njaa. Alizingatia mambo ya mazingira maanani na kuona sehemu mbalimbali ambazo zinaweza kuwasaidia wananchi wake. Leo hii tunasema maji ni uhai. Lakini, bila mito yetu kuwa dhabiti hatuwezi kupata chakula cha kulisha watu wetu kwa njia nzuri. Hali ya maisha imekuwa ngumu. Watu wengi sana wanagura kutoka mashambani kuja kwenye miji ili kutafuta kazi waweze kujikimu kimaisha. Hatuwezi kuishi mijini bila pesa mifukoni. Lakini, kule mashambani tukiifadhi mito yetu na mazingira tutaweza kuwa na chakula cha kutosha yaani food security . Ninafikiri hapo sijachanganya lugha sana isije Hon. Tandaza akaruka tena. Ninamwamia sana kwa sababu wakati fulani aliniwakilisha kwenye eneo Bunge langu sawa sawa na akajigeuza kama fulangenge. Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie. Ninataka kuingia kwenye rekodi za Bunge kuwa ninasimama kumuunga mkono Mhe. Irene Mayaka. Ahsante. Mungu akubariki."
}