GET /api/v0.1/hansard/entries/1499486/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1499486,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499486/?format=api",
"text_counter": 349,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii ya kuchangia Mswada huu. Mazingira ni kila kitu. Katika taifa lenye afya na nguvu, ni lazima mazingira yapewe kipaumbele ili vitu vingine vipatikane. Ninamuunga mkono na kumshukuru Mhe. Mayaka kwa kuuleta Mswada huu wa kuyalinda mazingira. Kama nilivyosema hapo awali, mazingira ni muhimu. Hata kama mti wa mkalatusi una faida zake, pia una madhara yake. Ni vyema kulinganisha faida na hasara ya kitu ili kujua ni ipi imezidi. Kama vile Mhe. Mayaka alivyotaja, huo mti unakausha maji kwenye mito na kutoa nguvu kwenye mchanga. Hiyo ni hasara kubwa kwa taifa. Kwa hivyo ni vyema kuondoa mti huo kabisa ili usipatikane katika maeneo yetu. Kuna Wabunge ambao wamesema kuwe na sehemu maalum ambapo mti huo utapandwa kando na mito. Siyo kwamba ninapinga maoni yao, lakini kama mti huo unanyonya maji, basi hata ukipandwa katika sehemu fulani, bado utanyonya maji katika sehemu ambazo maji yanatembea chini ya ardhi na kusababisha madhara ya sehemu hizo kukauka. Hii ni kwa sababu kuna maji yanayopita chini ya ardhi na huenda katika sehemu fulani. Yana faida kubwa katika taifa. Mti huo ukishakausha sehemu hizo, ardhi haitakuwa na nguvu. Kuna sehemu nyingi ambapo ijapokuwa huoni madhara ya mti huo waziwazi, kuna madhara ya mbali. Kwa mfano, mti huo haukubali mimea kumea ama unafanya chakula kinakosa rutuba kwa sababu umenyonya maji yote. Tumeona pia kampuni ya Kenya Power ikiutumia mti huo. Ni vyema waje na mbinu mbadala ili isiwe lazima watumie mti huo. Ni heri hata watumie saruji kusimamisha nguzo zao ili miti hiyo ipigwe marufuku kabisa. Ikiwa ni lazima ipandwe, basi ni vyema iwe katika fuo za bahari. Pale baharini, kuna miti inayoitwa mikoko ambayo mara nyingi humea yenyewe. Ikiwa ni lazima mti wa mkalatusi upandwe ilhali unanyonya maji kwa wingi, basi upandwe baharini ili unyonye maji yaliyo baharini kwa sababu hayawezi tokomea. Maji katika bahari ni"
}