GET /api/v0.1/hansard/entries/1499488/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1499488,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499488/?format=api",
    "text_counter": 351,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": "mengi. Kwa hivyo, mti huo upandwe kando ya bahari lakini sio katika ardhi ambayo tunategemea maji yaliyomo chini ya ardhi. Nimesimama kuuunga mkono Mswada huu na kuhakikisha kuwa mti huo uondolewe. Ingawa wakati uliletwa nchini ulifanyiwa utafiti, kila siku utafiti hufanywa duniani na kuna vitu ambavyo tulikuwa tunavitumia zamani lakini sasa havifai. Kwa mfano, zamani tulikuwa tukitumia asbestos lakini baada ya utafiti, ilisemekana kuwa inasababisha ugonjwa wa saratani. Vile vile, watu wameona kuwa mti huo wa mkalatusi una hasara kubwa. Kwa sababu hiyo, inabidi tuache kufanya vitu ambavyo tulikuwa tukifanya mwanzoni bila kujua. Utafiti wa kileo unatofautisha vitu vingine ambavyo havifai. Mti huo ni mojawapo ya vitu ambavyo havifai. Kwa hivyo, ninauunga mkono Mswada huu ili mti huo uondolewe na kuletwe mti mwingine utakaokuwa na manufaa. Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}