GET /api/v0.1/hansard/entries/1499496/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1499496,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1499496/?format=api",
"text_counter": 359,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "matusi”. Lakini mti huo tayari unaonyesha kuwa una balaa kwa sababu ukimzaa mtoto wako halafu unampatia jina kama “njaa” ama “taabu”, ushamlaani kuanzia pale mwanzo. Kwa hivyo, mti huo wa mkalatusi tayari una matusi, nuksi na balaa. Ndiyo maana umetufikisha pale ambapo tupo sasa hivi. Ukizingatia historia ya mti huo, ni wazi kuwa si wa kiasili. Uliletwa na mzungu katika karne iliyopita wakati walipokuwa wakijenga reli. Waliona kuwa hapakuwa na mbao za kutosha kwa hivyo wakaleta mti huo bila utaratibu, ufasaha, ama kufanya utafiti wa madhara yake. Kwanza, ieleweke kwamba huu sio mti ulioletwa kwa nia njema ama kwa kuzingatia hali yetu ya kimazingira. Ikiwa ni mti ulioletwa na saa hii unaleta madhara, basi hatustahili kuchukua muda mwingi kuuzungumzia huku tukijiuliza upandwe au uondolewe wapi. Mti huu hauwezi kufanya vizuri ukiupanda mahala ambapo hapana maji. Mti huu utahitaji maji ili unawiri mahali popote utakapopelekwa. Inamaanisha kuwa lazima upelekewe maji ikiwa utapelekwa sehemu isiyo karibu na mito. Je, maji haya yatatoka wapi? Hayatatoka Ulaya ulikotoka mti huo. Itabidi tutumie maji yetu. Hapo ndipo hatari inapoingia. Utafiti unaonyesha kwamba mti huu, ili unawiri, utahitaji kati ya lita sitini na mia mbili za maji kila siku. Hata binadamu hahitaji maji kama haya. Hili ni jinamizi au jini lililokuja kutumalizia maji na mazingira yetu. Hatimaye, litatuangamiza tubaki na mkalatusi ulio na matusi ndani yake. Katika sehemu ninayotoka ya Kwale, mti huo sanasana ulipandwa karibu na kinamasi au swamp kwa Kimombo. Hii ni ili nisiwe nazungumza na sieleweki nasema nini. Tulikuwa tukipanda mpunga. Kwa Kiswahili, ieleweke kwamba hatupandi mchele ila mpunga. Mchele huja baadaye. Hatuna tena zao la mpunga sehemu niliyozaliwa ilhali tulikula vizuri wakati huo. Hii ni kwa sababu mti huo umekausha maeneo yote yaliyokuwa na kinamasi. Sehemu nyingi nchini tunatumia maji kutoka kwa mabwawa kwa sababu mifereji haijafika kila mahali. Mti huu hukausha ardhi unapopandwa sehemu za mabwawa. Mabwawa nayo kukauka, husababisha madhara makubwa kwa binadamu na wanyama ambao wangetumia maji hayo. Mti huu hubaki kuwa nuksi hudhalilisha maisha yetu. Endapo mti huu utapandwa sehemu iliyo na kisima, basi kitakauka. Kikikauka, tunajua madhara yanayotokea. Huu mti hautufai. Tulikuwa na miti yetu ya kiasili. Kule kwetu tungepanda miti kama mikwakwa, mizaje, mininga, mikwaju, na kadhalika. Miti hii haikuwa na madhara yoyote. Pia, miti hii ingetumika kwa kazi nyingine zote ambazo mkalatusi hauwezi kutumika. Mara nyingi wenzetu tunaowaita marafiki kutoka ughaibuni hutupotosha na kutusababisha kuwacha mila, asili, na miti yetu. Walituletea miti ambayo eti inakua kwa haraka bila kutuambia madhara yake. Baadaye, sisi huhangaika na kurudi kwao kuomba misaada ili watutafutie utaalam ilihali wao ndio walioharibu mazingira yetu wakijua madhara ya miti hiyo. Kwa wale waliishi sehemu za Pwani miaka ya sabini na themanini, kulikuwa kunanyesha mvua kila asubuhi mjini Kwale. Usingekosa mvuke ambao kwao ungesikia miti ikivuma kwa unyevunyevu uliokuwa pale. Hakuna hilo tena. Hili ni janga kubwa. Ni sehemu nyingi sana za nchi hii ambazo zimeathirika. Nikiunga Mswada huu mkono, ninatoa kongole zangu kwa mwenzetu, dada yetu, Irene ambaye ameuleta. Nisisitishe tu kwa kuunga mkono. Ningetaka kumuunga hata mguu ili Mswada huu utiliwe maanani haraka iwezekanavyo. Janga hili litatuathiri sote na kutuangamiza ilihali tuna uwezo."
}